Mkono wa pole - Kifurushi cha NURU (Watu 6):
Hii ni bima ya maisha inayotoa mkono wa pole kwa mwanachama, familia ya mwanachama ya watu sita (mwanachama, mwenzi wake, na watoto hadi wanne).
Mwanachama akilipia TSh6,000 kwa mwaka atafidiwa kiasi cha TSh1,000,000 kwa mwanafamilia yoyote ambaye atapoteza maisha.
Kiasi hiki cha TSh1,000,000 kitalipwa kwa mwanachama au familia yake kupitia ofisi za CHAMWAPITA zilizoko kwenye mkoa husika.
Bima hii ni kwa ajili ya majanga ya kifo pekee. Hivyo italipwa kwa mwanachama au familia yake pale ambayo mwanachama amepoteza maisha au mmoja wa wanafamilia ya mwanachama amepoteza maisha.
Jumla ya kiwango kitakachotolewa kwa mwanachama au mwanafamilia ya wamachama anapokuwa amepoteza maisha ni kiasi cha TSh1,000,000 tu.
Mashari na vigezo vinavyohitajika ni hivi:
- Mwanachama awe na umri kati ya miaka 18 hadi 65
- Mwanachama awe kitambulisho cha kura au cha taifa au cheti cha kuzaliwa
- Mwenza wa mwanachama awe kitambulisho cha kura au cha taifa au cheti cha kuzaliwa
- Watoto wa mwanachama wawe na cheti cha kuzaliwa
- Watoto wa mwanachama wanaotambulika ni wale wenye miaka isiyozidi 21
- Mwanachama awe amesajiliwa kwenye mfumo huu wa CHAMWAPITA na kulipia ada ya kujiandikisha (TSh3,500), ada ya chama ya mwaka (TSh1,000), gharama ya bima ya TSh6,000
Mkono wa pole - Kifurushi cha NURU YA WAZAZI (Watu 10):
Hii ni bima ya maisha inayotoa mkono wa pole kwa mwanachama, familia ya mwanachama ya watu sita (mwanachama, mwenzi wake, na watoto hadi wanne), wazazi wa mwanachama (baba na mama) na wazazi wa mwenza wa mwanachama (wake- baba na mama).
Mwanachama akilipia TSh24,000 kwa mwaka atafidiwa kiasi cha TSh1,000,000 kwa mwanafamilia yoyote ambaye atapoteza maisha.
Kiasi hiki cha TSh1,000,000 kitalipwa kwa mwanachama au familia yake kupitia ofisi za CHAMWAPITA zilizoko kwenye mkoa husika.
Bima hii ni kwa ajili ya majanga ya kifo pekee. Hivyo italipwa kwa mwanachama au familia yake pale ambayo mwanachama amepoteza maisha au mmoja wa wanafamilia ya mwanachama amepoteza maisha.
Jumla ya kiwango kitakachotolewa kwa mwanachama au mwanafamilia ya wamachama anapokuwa amepoteza maisha ni kiasi cha TSh1,000,000 tu.
Mashari na vigezo vinavyohitajika ni hivi:
- Mwanachama awe na umri kati ya miaka 18 hadi 65
- Mwanachama awe kitambulisho cha kura au cha taifa au cheti cha kuzaliwa
- Mwenza wa mwanachama awe kitambulisho cha kura au cha taifa au cheti cha kuzaliwa
- Watoto wa mwanachama wawe na cheti cha kuzaliwa
- Watoto wa mwanachama wanaotambulika ni wale wenye miaka isiyozidi 21
- Mwanachama awe amesajiliwa kwenye mfumo huu wa CHAMWAPITA na kulipia ada ya kujiandikisha (TSh3,500), ada ya chama ya mwaka (TSh1,000), gharama ya bima ya TSh24,000